alipokea taarifa ya eneo la uwakilishi la Ubalozi ambalo linajumuisha Afrika Kusini, Botswana, Falme ya Lesotho na SADC. Taarifa hiyo ilieleza juhudi za Ubalozi katika kukuza mahusiano na nchi za eneo la uwakilishi, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa diplomasia ya uchumi, diplomasia ya siasa, wanadiaspora wa eneo la uwakilishi. 

Mhe. Waziri alipokea taarifa hiyo na kupongeza Ubalozi kwa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi na kwa maslahi ya Taifa. Pamoja na mambo mengine, Mhe Waziri Mulamula alisema kwa vile huu ni Ubalozi wa kwanza ameutembelea tangu uteuzi wake kwa nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Hivyo ameutaka Ubalozi kuendela kufanya kazj kwa malengo, watumishi kujiwekea malengo binafsi ili kufanikisha malengo ya Ubalozi na hatimaye Ubalozi kuchangia malengo ya Wizara kwa ujumla.

Aliupongeza Ubalozi kwa utunzaji mzuri wa majengo kwa fedha ndogo wanazozipata. Aidha, Mhe Waziri ameutaka Ublozi kuendeleza mahusiano na nchi za uwakilishi na Balozi zingine zilizopo katika nchi za uwakilishi na suala hili la kujenga mahusiano na watumishi wote na siyo Balozi pekee yake. 

Mhe. Waziri aliongeza kwa kusema kuwa Ubalozi uangalie fursa za mafunzo kwa wtumishi yaani watumishi kushiriki kozi fupi kwa nia ya kuwajengea uwezo watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi Zaidi katika tasnia ya diplomasia. Mwisho, aliushukuru Ubalozi kwa mapokezi mazuri.