Tarehe 29 Aprili, 2026 Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb), Waziri wa Nishati ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na kukutana na Watumishi. Mhe. Waziri Ndejembi (Mb) na Ujumbe wake wapo nchini Afrika Kusini kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Umoja Afrika wanaosimamia Miundombinu na Nishati,utakaofanyika jijini Johannesburg tarehe 30 Aprili, 2026.
Wakati wa mazungumzo Ubalozini, Mhe. Ndejembi (Mb) amewakaribisha Wawekezaji kutoka Afrika Kusini kwenda kuwekeza nchini Tanzania katika uzalishaji wa nishati ya Umeme kutoka Makaa ya Mawe, kama inavyofanyika nchini Afrika Kusini.