Tarehe 30 Aprili, 2026 Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umewaongoza Wanadiplomasia na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa nchini Afrika Kusini kusherehekea Miaka 62 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Hafla ya maadhimisho hayo ilihudhuriwa naMabalozi kutoka nchi mbalimbali; Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa; Viongozi wa Jumuiya za Watanzania nchini Afrika Kusini; pamoja na Watu Mashuhuri, akiwemo Mwanamuziki Bi. Yvonne Chakachaka pamoja na Bw. Sipho Mabuse (Hotstix), Mtunzi wa wimbo maarufu wa 'Zanzibar beautiful Island of Africa'.

Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Mkhuleko Hlengwa (Mb); Naibu Waziri wa Uchukuzi - kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini. Ameishukuru Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake kwa Afrika Kusini, wakati wa Ukombozi, na kwa kuwa mbia muhimu wa biashara wa Afrika Kusini, Barani Afrika.