Tarehe 25 Mei, 2026, Mhe. Balozi James G.Bwana, amefanya Mkutano na Wawakilishi wa Kampuni ya MACER WINGS ya Ufaransa pamoja na AVES HOLDINGS ya Afrika Kusini katika Ofisi za Ubalozi Jijini Pretoria.Kupitia Mkutano huo, Makampuni hayo mawili yamewasilisha dhamira yao ya kutoa huduma ya matengenezo ya Vyombo vya Usafiri wa Anga vilivyopo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kushirikiana na Mamlaka za Tanzania katika Sekta ya Usafirishaji wa Anga.