Tarehe 12-14 Mei, 2026, Ubalozi pamoja na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo kutoka nchini Tanzania, walishiriki Maonesho ya NAMPO HARVEST DAY nchini Afrika Kusini, yaliyoandaliwa na GRAIN SA. Maonesho hayo ni miongoni mwa maonesho makubwa ya kilimo barani Afrika na yaliwaunganisha Wakulima (wakubwa, wa kati na wadogo), Wataalam wa kilimo na mifugo, Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali kutoka Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla.
Pamoja na masuala mengine, Ubalozi ulitumia fursa hiyo kuwatangazia Wadau fursa mbalimbali za kilimo zilizopo nchini Tanzania na kuwahamasisha kushiriki katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam - DITF) yatakayofanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2026 katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, pamoja na Maonesho ya Kimataita ya Kilimo ya Nanenane yatakayofanyika tarehe 1-8 Agosti, 2026.