Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, ametembelea Ubalozi wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Jenerali Mabeyo yupo nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kumuaga Mkuu Majeshi wa Afrika Kusini Jenerali SZ Shoki zilizofanyika kitaifa Mei 28 Mjini Pretoria.

Kuhudhuria sherehe hizo ni utaratibu uliowekwa  na nchi wanachama wa Jumuiya za SADC ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuimarisha mashirikiano hususan katika nyanja ya Diplomasia ya Ulinzi (Defence Diplomacy) na Amani katika eneo Ia nchi za SADC.

Jenerali Mabeyo, alikaribishwa Ubalozini na Balozi Mej. Jen. Gaudence Milanzi (Mst) na watumishi wa Ubalozi, Balozi Milanzi alitoa taarifa fupi ya eneo la uwakilishi ya Afrika Kusini, Botswana na Falme ya Lesotho.

Balozi alieeza kuwa hali ya uwakilishi inaridhisha kiulinzi na kiusalama, Ubalozi umeendelea kukuza mashirikiano na nchiza eneo la uwakilishi ikiwa ni pamoja na SADC, kwa kufuata miongozo ya sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania inavyoelekeza kuendeleza Diplomasia ya kisiasa na kutekeleza Diplomasia ya uchumi.

Upande wake Jenerali Mabeyo alielezea ziara yake kwa ujumla nchini Afrika Kusini imekuwa ni ya mafanikio na pia kuna mambo kama Mkuu  wa Majeshi ameona yanafaa kuigwa ili kuboresha utendaji wa Jeshi la Tanzania.

  • Kikao kikiendelea kati ya CDF Mabeyo na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Afrika ya Kusini
  • CDF Mabeyo katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi