Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika kuendeleza na kuimarisho ushirikiano wa nchi hizo mbili viongozi hao wamependekeza kufanikisha ziara ya Mhe. Waziri Mulamula nchini Finland pamoja na ushiriki wake katika mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Nordic utakaofanyika nchini Finland mwezi Juni 2022. 

Katika mazungumzo ya viongozi hao, Balozi Mulamula amemhakikishia Balozi Swan kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Finland katika kuhakikisha Mataifa hayo yanashirikiana kijamiii, kisiasa na kiuchumi.

"Finland amekuwa mdau Mkubwa wa Maendeleo hapa nchini kwetu hasa katika sekta ya fedha hususan katika masuala ya kodi, mazingira, tehama, uongozi pamoja na uwezeshaji wa wanawake.

Katika mazungumzo yangu na Balozi wa Finland tumekubaliana kuendeleza ushirikiano wetu kwa Maendeleo endelevu," amesema Balozi Mulamula.
Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbink Tanzania Bw. Kevin Wingfield